mkapa 4

Buriani Mkapa! marehemu rais mstaafu wa Tanzania azikwa leo

Marehemu rais mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa anazikwa leo Jumatano nyumbani kwake katika kijiji cha Lupaso, wilaya ya Masasi mkoani Mtwara, Kusini mwa nchi ya Tanzania.

Mkapa aliaga dunia usiku wa Alhamisi akiwa hospitalini alikokuwa amelazwa akipokea matibabu. Rais John Pombe Magufuli alitangaza kupitia runinga ya taifa taarifa za kufariki dunia kwa kiongozi huyo wa awamu ya tatu katika hospitali moja jijini Dar es Salaam.

Soma habari zaidi;

Tanzia! rais mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa aaga dunia

Nchi hiyo imekuwa ikiendelea na maombolezi ya siku tatu mfululizo katika hafla ya kitaifa ilioanza siku ya  Jumapili.

Marehemu Benjamin Mkapa
Marehemu Benjamin Mkapa

Kuanzia hiyo Jumapili wananchi wamekuwa na fursa ya kumpa heshima ya mwisho aliyekuwa rais wao aliyehudumu kati ya mwaka 1995 – 2005.

Soma habari zaidi;

Kenya yakanusha madai ya ndege yake kuzuiwa kutua Tanzania

Mkapa alikuwa rais wa tatu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania na alichukuwa usukani kutoka kwa Ali Hassan Mwinyi ambaye alikuwa amechukuwa majukumu hayo kutoka kwa rais mwanzilishi wa taifa hilo hayati Mwalimu Julius Nyerere.

 

 

Mzee Mkapa alizaliwa Novemba 1938, katika mkoa wa Mtwara kusini mwa Tanzania, na aliliongoza taifa la Tanzania kwa mihula miwili kabla ya kustaafu na kumuachia mamlaka Jakaya Mwisho Kikwete.

Photo Credits: Maktaba

Read More:

Comments

comments