Asema yeye na DJ Mo hawatakiswi na lolote sasa

Ati? Size 8 anasema ni habari njema kwamba DJ Mo alitoka nje ya ndoa ,amefurahia matokeo

Sakata hiyo nusura iivunje ndoa yao

Muhtasari

 

  • "Sasa tuko pamoja kwa uthabiti hata kuliko zamani" Size 8 asema 
  • DJ Mo ameonekana kusononeshwa na kitendo chake na amesamehewa 
  • Nilimpenda vile yesu alinipenda-Size 8 

 

Pamoja:Size 8 na DJ Mo

 Msanii Size 8 amezungumza kuhusu sakata ya mume wake DJ Mo kutoka nje yandoa na mwanamke mwingine kwa jina Margaret Wanyama.

 Katika kipindi chao cha kila wiki,Dinning with the  Murayas  Size 8  amesema amefurahi kwamba sakata hiyo ilifichuka kwani sasa yeye na mume wake wamekaribiana sana na kujenga hata zaidi uhusiano uliopo kati yao.

 Amesema  aliamua kusimama na mume wake kwa sababu awali naye pia alikuwa mtenda dhambi lakini Yesu anampenda na hivyo basi hakuwa na budi ila kumsamehe DJ Mo.

 

 Anasema amefurahia matokeo ya sakata hiyo nzima kwani iliwaleta karibu sana  kama wanandoa na wamefanya maombi pamoja na hata kufunga. Amesema ndoa yao wakati huu ipo thabiti kuliko ilivyokuwa hapo awali.

 Size 8 amesema wanamitandao hawawezi kuelewa mbona hakuchukua hatua kali kama vile kumkemea mume wake kuhusu kilichotokea.

"…Watu wengi hawakuelewa  ama kuamini nilichofanya kwani walifikiri ningeitumia fursa hiyo kumshtumu DJ Mo na kuzitupa nguo zake. Sikutaka jambo hilo kuvunja ndoa yetu kama alivyotaka shetani" amesema Size 8.

 Aliongeza ;

 "Nilimuangalia nikasema, nataka  kumpenda jinsi Kristu alivyonipenda, alipatwa na mshtuko pia yeye".

DJ Mo  naye alisema

“Kuna vitu ambavyo watu hawavijui, vipo ndani ya pazia. Tuliwacha kuposti kila mmoja katika mitandao ya kijamii kwa wiki tatu na watu wakafikiri tumeachana. Alikuwa nami wakati wote wa dhoruba hilo".

(Mhariri Davis Ojiambo)