Mchekeshaji Othuol Kuzikwa Jumamosi huku wasanii wakitarajiwa kuchanga shillingi elfu 700

Muhtasari

Kifo chake mchekeshaji Othuol

wasanii kuchanga mchango wao ili kugharamia mazishi yake

Othuol Othuol
Image: hisani

Tasnia ya ucheshi,mashabikii wakenya a jamaa wa jmla wanaomboleza kufuatia kifo cha mchekeshaji tajika na muigizaji maalum Ohuol Othuol aliyeaga wikendi iliyopita baada ya kuugua kwa muda.

Kwa ushirikiano, wasanii pamoja na mashabiki wa marehemu wanatarajia kuchanga kati ya KSh 700,000 na milioni moja ambazo zitagharamia mazishi ya mchekeshaji huyo.

Kulingana na taarifa kutoka kwa mwenyekiti wa Comedians in Kenya Society Ken Waudo, fedha hizo zitagharamia vifaa na kila kitu kitakachohitajika kwa ajili ya kumpea marehemu heshimu zake za mwisho.

 

" Maandalizi ya mazishi ya Othuol Othuol yanaendelea, marehemu anatarajiwa kuzikwa Jumamosi, Oktoba 24 nyumbani kwao kijijini Ndere, eneo bunge la Asego kaunti ya Siaya

Othuol-34-1-1
Othuol-34-1-1

" Tunapanga kuwa na mchango wa kifedha , tutawatangazieni ni lini, fedha hizo zitatumika kugharamia mazishi ya mwendazake." Waudo Alizungumza.

Je marafiki wa kweli ni akina nani watakao fanikisha siku hiyo kupitia kwa mfuko wao? mwendazake alikuwa anaugua uvimbe wa ubongo huku akiaga akipokea matibabu katika hospitali ya Kenyatta.