Margaret Wanyama asema hajali

Sijali! Mwanamke aliyedai kuwa mpenzi wa DJ Mo asema huku Size 8 na DJ Mo wakiambiana maneno matamu

Size 8 asherehea ushindi wa kusawazisha mambo na DJ Mo

Muhtasari

• Margaret Wanyama asema hajali 

• Size 8 asherehea ushindi wa kusawazisha mambo na DJ Mo

• Wawili hao wanaadhimisha miaka 7 ya ndoa yao 

 

Margaret Wanyama

 Ndoa ya Size 8 na DJ Mo imepitia majaribu katika siku chache zilizopita baada ya Margaret Wanyama kujitokeza na madai kwamba alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na DJ Mo.

 Kila jambo lilionekana kana kwamba litasimama katika maisha ya ndoa ya wawili hao lakini Hapana!

The murayas wamesimama kidete katika mapenzi yao na kulingana na jumbe ambazo wametumiana katika mitandao ya kijamii mambo bado ni kweli Size 8 alifunga sala  ili kuiokoa ndoa yake .

 
 

 Aliyetangulia kutuma ujumbe  wa kuonyesha msimamo ni DJ Mo huku akimsifu Size 8  kama "mama ya watoto wangu na Malkia wangu".  Aliongeza kusema kwamba wamepitia mengi naye haogopi kukabiliana na changamoto zaidi katika ndoa yao.

 Size 8 naye aliandika ujumbe kuhusu jinsi  Mapenzi yanashinda vita dhidi ya uongo na uvumi. Katika ujumbe huo ambao pia alimshirikisha mume wake DJ Mo, Size 8 aliashiria kwamba yote wanayopitia  yatakwisha.

 Sasa kilichowavuta wengi macho ni jibu la Margaret Wanyama ambaye yupo katikati ya patashika nzima hii. Wanyama alituma ujumbe fiche kupitia njia ya  wimbo wa video uliokuwa na  maneno kama "I don’t care". Yamaanisha kwamba hajali kuhusu kinachofanyika upande wa pili baada ya DJ Mo kuonekana kupata msamaha wa mke wake. Mambo haya!

(Mhariri Davis Ojiambo)