Mwanasosholaiti Shakilla azungumza baada ya kuachiliwa na kusema haya

Muhtasari

•Mwanasosholaiti aachiliwa kwa dhamana baada ya msanii Willy Paul kumripoti

•Tulikuwa tunajuana lakini niliwekwa kwa mtego

 

Willy paul na shakilla
Image: hisani

Mwanasosholaiti Shakilla hatimaye aliweza kuachiliwa huru huku akizungumza na kusema kuwa msanii Willy Paul alidanganya kwa kusema kuwa alijilazimisha nyumbani kwake ilhali alikuwa amemualika.

Jumanne asubuhi Willy kupitia kwenye mitandao yake ya kijamii ya instagram aliandika ujumbe na kueleza vile kisa hicho kilitokea huku Shakilla akipinga madai hayo.

Baada ya Shakilla kutoka korokoroni aliandika haya.

 

"Nimeachiliwa kwa dhamna lakini nina habari ya kuwaambia,inayopendeza wacha nile na nitoe machungu yote

Sijawahi hisi kuharibiwa na kudanganywa kama Jana mtu kukupigia simu vizuri huende kwake vyema mahali ambapo unafafahamu na sisi sote tunafahamu lakini mtu anakuweka kwa mtego kwa kujilazimisha kuingia kwake kama wtf???

Nina mengi ya kusema lakini ngojeni ukweli,nimewekwa wa mtego na si vyema nitakuwa mtu mkubwa huku." Shakilla Aliandika.

Huku msanii Paul akieleza aliwaambia mashabiki wamuombee pamoja na familia yake kwa maana hwayuko salama.