Orodha ya wachekeshaji walioaga dunia bado wakifanya kazi yao ya ucheshi

Muhtasari

•Wachekeshaji walioaga dunia

•Vifo ambavvyo vilishtua wengi

•Wacheshi ambao walipendwa na wengi

•Sababu ya vifo vyao

Wacheshi
Image: Hisani

Kumpoteza umpendaye ni jambo ambalo si rahisi kukubali hasa moyoni mwako kwa maana ameenda na amekuacha milele hadi pale mtkutana tena mbinguni.

Tasnia ya ucheshi na burudani humu nchini iliwapoteza na inazidi kuwapoteza wachekeshaji wa humu nchini kwa njia tatanishi na wengine wakiugua na kisha kupumua pumzi yao ya mwisho.

Wengi waliaga na wameaga kbla ya kutimiza maazimio yao ya maisha hasa ya kuweka tabasamu usoni mwa wananchi na mashabiki wao.

 

Hivi majuzi mchekeshaji wa churchill show Othuol Othuol aliaga dunia huku mashabiki na wakenya wakiwalaumu maceleb na usimamizi wa tasnia hiyo kwa kutoonyesha usaidizi wao.

Hii hapa orodha ya wachekeshaji walioaga dunia bado wakiwa kazini mwao ya ucheshi.

1.Papa Shirandula

EdNONYNWoAQuvo1
charles bukeko EdNONYNWoAQuvo1
Image: hisani

Muigizaji huyo na mcheshi Charles Bukeko kifo chake kiliwashtua wengi huku wengi wakibaki na maswali mengi kuliko majibu.

Papa aliaga dunia mnamo JUlai,18,2020 baada ya kuugua virusi vya corona.

2.Nancy Nyambura(Jastorina)

Kipindi cha Nancy kilikuwa kinafahamika kama Jastorina na ambacho kilipeperushwa katika runinga ya Citizen kila jumamosi.

Mchekeshaji huyo aliaga dunia 30,Juni 2020 baada ya kupata maumivu ya kichwa, huku wengi wakitazamia kumuona tena katika uigizaji wake bali ndoto zao zilizimwa baada ya yake kuaga dunia

3.Othuol Othuol

Ni kifo ambacho tasnia ya burudani imekumbana nayo hivi majuzi huku mchekeshaji huyo akiaga dunia baada ya kuugua uvimbe wa kichwa

Othuol-34-1-1
othuol othuol Othuol-34-1-1
Image: hisani

Othuo amekuwa ndani na nje ya hospitali kila mara ili aweze kutibiwa na kuendelea na kazi yake lakini kazi yake ilikatizwa kwa ufupi baada ya kupumua pumzi yake ya mwisho.

4.Njenga Mswahili

Ni mcheshi ambaye alikuwa ametazamiwa sana na mashabiki wake, Njenga alisongwa na mawazo na kisha kupatikana akiwa ameaga dunia mnamo Novemba mwaka janga huku kiini cha kifo chake kikijulikana kama aligongwa na gari moshi

5.Emmanuel Makori

Mchekeshaji Ayeiya aliaga dunia baada ya kuhusika katika ajali ya barabara mnamo mwaka wa 2017.

Miongoni mwa wachekeshaji wengine walioaga dunia bado wakifana kazi yao ni pamoja na mzee Ojwang,Kasee miongoni mwa wengine.

Kutoka kwetu wanajambo Mungu azidi kulaza roho zao mahali pema peponi.