'Othuol aliamua kuvalia suti ya kijani ili kunishukuru,'Jalang'o akana madai haya

Muhtasari

•Othuol aliamua kuvalia suti ya kijani ili kunishukuru kwa yale nilimtendea

•Tumekuwa tukimsaidia Othuol kutoka wakati wa kwanza alipokuwa amelazwa hospitalini 

•Kama mmeamua kinishirikisha katika mawazo yenu mimi ni nani wa kuyabadilisha

Jalang'o
Jalang'o Jalang'o
Image: Hisani

Mtangazaji Jalang'o amejitenga na kukana madai ya kuwa alimnyima mwendazake mchekeshaj Othuol elfu 15 alipokuwa anazihitaji.

Huku akikana madai hayo kupitia kwenye ukurasa wake wa facebook alikuwa na haya ya kusema;

"Kwa hivyo mwanablogu mmoja aliamka na kuamua kuwa screenshoti ya Othuol akihitaji elfu 15 ni mimi unaona siku hizi nimezoea kushirikishwa kwa kila jambo

 
 

niliamka na kuona hii blogu ikisema kuwa 'Vile Jalango alimkataza Othuol elfu 15' woow je wajua vile unaweza kukaa chini na kushindwa nini ulichowakosea watu lakini nimezoea sasa na hainisumbui huwa wanatafuta jinsi ya kukushusha chini." Aliandika Jalang'o.

Screenshot_from_2019_11_16_12_22_42__1573896949_82740
Screenshot_from_2019_11_16_12_22_42__1573896949_82740

Mtangazaji huyo alisema ya kwamba walifanya harambee tatu ili kumsaidia Othuol kabla ya kifo chake huku wakiwa wameongozwa na muigizaji Sandra Dacha.

"Katika kikundi cha comedians kenya Sandra Dacha amekuwa akichukua pesa tangu siku ya kwanza Othuol alilazwa tumekuwa na zaidi ya harambee 3 pesa ambaz zimekuwa zikigharamia gharama yake tumekuwa hapo hadi dakika ya mwisho

Lakini ukiamua kunishirikisha katika screenshot hiyo na mawazo  yako mimi ni nani wa kuyabadilisha si mimi endelea na kunishirikisha 

Alafu uje katika kamati ya kupanga mazishi utuambie tukuongeze katika mipango hiyo, uhusiano wangu na Othuol Hutawahi badilika."

Aliendelea na kunakili ujumbe wake na kusema kuwa Othuol aliamua kuvalia suti ya kijani baada ya kumsaidia katika kazi yake kama ishara ya kumshukuru,

"Na kunishukuru aliamua kuvalia suti ya kijani kama mimi nitawaambia habari hiyo siku nyingine jinsi alivyopata suti yake ya kijani

 
 

kifo chake Othuol ni cha huzuni inauma sana, tulifanya tuwezalo mnaweza kosa kuelewa kwa sasa." Jalang'o Alinakili.