Hongera Grace Msalame ajifungua mtoto mvulana

Muhtasari
  • Grace Msalame ajifungua mtoto wa mvulana
  • 14 Oktoba itasalia kwa moyo wangu milele
60896847_373345770038247_8938989417775036920_n-696x696
60896847_373345770038247_8938989417775036920_n-696x696

Mtangazaji Grace Msalame hii leo ameweza kutangaza kujifungua kwake kwa mwanawe wa watatu hii ni baada ya kupata mapacha.

Kupitia kwenye mitandao yake ya kijamii ya instagram Grace aliandika ujumbe baada ya kujifungua na kusema kuwa mwanawe anafahamika kama Isaiah.

Huku kupitia mitandao hiyo aliposti maua na kusema ya kwamba tarehe 14 Ocktoba itasalia moyoni mwake milele.

"Kwa mwanzo mpya mzuri, tarehe 14 Oktoba itasalia moyoni mwangu milele #BabyIsaiah👶🏽 #GloryToGod🙏🏾." Aliandika Msalame.

Kujifungua kwake kunajiri baada ya miezi mitatu kutangaza kuwa ni mjamzito na ujauzito wake ni wa miezi sita huku ukiwa kwenye siri miezi hiyo nyingine yote.

Marafiki na mashabiki wake alimtumia jumbe za kumpongeza baada ya wao kuona ujumbe wake Grace.