Nilikuwa nataka kujiua, sijawahi jiona kama mtu mashuhuri-Azziad Nasenya

Muhtasari
  • Sijawahi jiona kama mtu mashuhuri mimi ni mtu wa kawaida
  • Nilifuta akaunti yangu twitter
  • Nina meneja ambaye amekuwa katika hii tasnia kwa muda mrefu
  • Huwa naomba Mungu ili niwe mnyenyekevu

Muigizaji na malkia wa Tiktok Azziad Nasenya akiwa kwenye mahojiano alisema kuwa hajawahi dhani kuwa ataweza kuwa mtu mashuhuri kando na hayo baada ya kuvuma sana baada ya kufanya challenge ya wimbo wa 'Utawezana' alipokea kejeli na ukosoaji mwingi sana huku akisema kuwa alikuwa anataka kujiua.

Pia Azziad alisema kuwa huwa anamuomba Mungu kwa unyenyekevu kila mara, alidai kuwa hawezi sema kuwa yeye ni mnyenyekevu bali anawaachia watu na mashabiki kuamua hayo.

Alisema kuwa huwa anajiona kama Azziad Nasenya na wala si mtu mashuhuri , na wala hapendi kupatana na watu na kumuona kama mtu mashuhuri.

 

femi 5
femi 5
 

"Sijawahi fikiria kama mimi ni celeb, huwa namuomba Mungu kwa unyenyekevu sitajibu kama mimi ni mnyenyekevu hiyo ni kazi ya watu kusema

Lakini kwangu mimi sijawahi jiona kama celeb huwa najiona kama Azziad na sipendi kila mahali niendapokila mtu anaiona kama celeb mkubwa mimi ni mtu wa kawaida." Alisema Azziad.

Alisema kwamba ilifika wakati akafuta mtandao wake wa kijamii wa twitter kwa ajili ya wakosoaji wake.

"Nilipoana nilikuwa na jambo fulani akilini mwangu, nilikuwa na kazi yangu ya kutia bidii kila siku na mambo mengine

Kwa hivyo sikupoteza hayo na pia nina meneja ambaye amekuwa katika tasnia hii kwa muda mrefu alinipa ushauri na kuniambia ni chukie maoni na nisiyajibu

Hivi ndivyo utaendelea jipe umuhimu wako nilifuta akaunti yangu ya twitter hadi leo sina kwa maana nina mambo ya maana ya kufanya." Alisema Azziad.

Kwa sasa Azziad anaigiza katika kipindi cha Selina kina chopeperushwa katika runinga ya Maisha Magic East.