'Mungu ametenda tena,'Msanii Kambua atangaza ujauzito wake wa pili

Muhtasari
  • Mungu ametenda tena kambua asema baada ya kutangaza habari njema
kambuacutepregdress
kambuacutepregdress

Msanii wa nyimbo za injili na mtangazaji Kambua ni hakikisho kuwa Mungu akipanga kukubariki kwa kweli atakubariki na hamna mwanadamu yeyote ambaye atazuia.

Kambua kabla ya kupata ujauzito wake wa kwanza alipokea kejeli nyingi na ukosoaji mwingi sana kutoka kwa watu tofauti.

Mungu aliwanayamazisha baada ya kubarikiwa na mwanawe wa kwanza.

 

Kupitia kwenye mitandao ya kijamii Kambua aliposti picha akiwa mjamzito kwa mara ya pili na kuandika ujumbe ufuatao.

"Mungu wa Sarah Mungu wa Hannah, Mungu wa Kambua punde tu nilipodhani umetenda mengi na ya kutosha Umetenda tena." Aliandika Kambua.

Baada ya mashabiki na marafiki zake kuona ujumbe wake Kambua walimpongeza na hizi haya baadhi ya jumbe zao.

sowairina: And she shares the Amazing news🤗🤗🤗Ari ri ri ri🤗💛Congratulations again Mama Twins😉We love you💛

Cate_actress: OMG baaaaabe CONGRATULATIONS 😭😭😭😭❤️❤️❤️❤️❤️🙏

revkathykiuna: Awwwwwww so beautiful. This God is too much . He’s a great God. Congratulations darling

sheilamwanyigha: God is amazinv🙌🏽🙌🏽🙌🏽🤗