Ukoo wetu unatutosha jamani,'Mama Dangote amshambulia Hamisa

Muhtasari
  • Mtu ulazimisha ukoo kweli mama dangote amuuliza Hamisa
  • Uko wetu unatutosha jameni
mama dangote
mama dangote

Hamisa Mobetto na mama yake msanii wa bongo Diamond Platnumz huwa hawaonani macho kwa macho wacha tu cheche za maneno ambazo huwa wanarushiana kwenye mitandao ya kijamii.

Siku chache zilizopita Hamisa alidai kuwa Diamond alihitaji DNA ili kuthibitisha kuwa mwanawe Dylan ni wake ambapo ripoti zilithibitisha ni wake.

Ugomvi wa wawili hao ulianza pale Hamisa alikuwa bado mpenzi wake Diamond, kuna wakati Mama Dangote alimpa Hmisa kichapo cha mbwa baada ya kumpatana na Diamond nyumbani kwake.

Haya basi baada ya mama Dangote kuona usemi wake Hamisa kupitia kwenye mitandao yake ya kijamii ya instagram alisema kwamba ukoo wao umewatosha na mtu halazimishi ukoo.

"Ukoo wetu unatutosha jamani!mtu analazimisha ukoo vipi? ebu nisaidieni kisheria ukoo unalazimishwa?" Mama Dangote aliandika.