'Umemwandalia meza machoni mwa watesi wake na kumpaka mafuta,'Kanze Dena ampongeza Kambua

Muhtasari
  • Mungu amemwandalia meza mbele ya watesi wake Kanze Dena ampongeza Kambua
  • Kambua alitangaza habari njema kupitia ukurasa wake wa instagram
Kambua

Msanii Kambua Manundu na mumewe Jackson Mathu wanatarajia mtoto wao wa pili, hii ni baada ya kubarikiwa na kifungua mimba wake mwaka jana na ambaye alifikisha mwaka mmoja Agosti mwaka huu.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram Kambua alitangaza habari njema  kuwa na ujauzito wa pili na kuandika ujumbe huu,

"Mungu wa Sarah na Mungu wa Hannah na mUngu wa Kambua punde tu nilipodhani kuwa umetenda ya kutosha umetenda tena." Aliandika Kambua.

 

Wasanii,wanahabari na mashabiki walimpongeza huku aliyekuwa mtangazaji wa runinga ya Citizen Kanze Dena akimpongeza na kusema kuwa Mungu amemwandalia Kambua meza mbele ya watesi wake.

Na huu hapa ujumbe wake Kanze Dena;

"Kila siku ....kila saa..Mungu umwaminifu...umemwandalia meza @kambuamuziki machoni mwa watesi wake na ukampaka mafuta..hakika wema nazo Fadhili zitamfuata dada na uzao wake siku zote za maisha yao.! JEHOVAH BABA MUNGU."Kanze Alinakili.