'Tunacheki drama kwa umbali,' Zari azungumza baada ya mama Diamond na Hamisa kukwaruzana mitandaoni

Muhtasari
  • Tunazickeki drama kwa umbali Zari azungumza baada ya haya kutokea
  • Ukoo wetu unatutosha Mama Dangote amshabulia Hamisa
  • Diamond alihitaji DNA ili kuhakikisha Dylan ni wake Hamisa afichua haya
zari
zari

Drama kati ya mama Diamond na Hamisa Mobetto inaonekana kumpendeza Zari Hassan, hii ni baada ya wawili hao kushambuliana kwenye mitandao ya kijamii

Haya yanajiri baada ya mama Dangote kumshambulia Hamisa na kumwambia kuwa ukoo haulazimishwi na kuwa ukoo wao unawatosha, hii ina maana kuwa alikuwa anajaribu kumwambia aache kujilazimisha katika familia yao.

Maneno yake Mama Dangote yalijiri pale Hamisa alidai kuwa Diamond aliitisha DNA ili kuhakikisha kuwa mwanawe Hamisa ni wake ambapo ripoti zilidhibitisha ni wake.

 

“Tukaenda tukapima DNA nadhani walichukua vipimo vinne kila mtu (mama, baba na mtoto) tukasign pale ivo wakasema tusubirie sijui ni 2 or 3 weeks so tukasubiria majibu yakatoka mtoto akatoka kwa asilimia zote ni mtoto wake na ikaishia hivyo. Na kwa kweli wakati tunaelekea hospitali alikuwa anajiskia vibaya. It was very sad for me to watch as a mother kwa sababu as a mother ni mimi natakiwa nijiskie vibaya."

Mama yake staa huyo wa bongo naye alikuwa na haya ya kusema;

"Ukoo wetu unatutosha jamani!mtu analazimisha ukoo vipi? ebu nisaidieni kisheria ukoo unalazimishwa?" Mama Dangote aliandika.

Zari amekuwa mama mwenye kupendwa na mama Dangote huku akijibu kuhusu majibishano hayo alikuwa na haya ya kusema.

"Vile tunazicheki drama kwa mbaaali."