Mambo ambayo mpenzi wako hapaswi kujua kukuhusu

Muhtasari
  • Mambo ambayo mpenzi wako hapaswi kufahamu kukuhusu
  • Mapenzi ni kama mmea lazima unyunyiziwe maji ili unawiri

Katika kila uhusiano wa kimapenzi lazima kila mmoja amwambie mpenzi wake siri zake na mambo ambayo amepitia kabla ya kukutana naye na kumkubali kama mpenzi wake wa maisha.

Ndio wakati huu wa sasa wengi hawadumishi uhusiano wao wa kimapenzi na kuacha mioyo ya wengi ikiwa imevunjika na kukata tamaa kwa maana hawangeamini ambacho walitendewa.

Lakini wengi ujiuliza ni wapi walikosea na ni nini walitenda ili kupita mateso ya kuumizwa mioyo.

Kuna mambo ambayo ukimpenda mtu hapaswi kufahamu kukuhusu, hata kama unampenda mpenzi wako unampenda vipi hapaswi kujua mambo haya ambayo nitanakili hapa chini kukuhusu,

1.Historia yako ya ngono

Kumpata mwanamke au mwanamume malkia ni ngumu sana hasa katika karne hii ya sasa, endapo umempata mpenzi wako usijaribu kumweleza kuhusu historia yako ya ngono au jinsi umalkia wako ulivunjwa.

2.Kuna mtu mahali ambaye anakupenda

Ndio kila mmoja anafanya kazi katika maeneo tofauti, lakini kama wajua kuna mwanamke au mwanamume katika sekta yako ya kazi ambaye anakumezea mate haya basi nyamaza na wala usimwambie ili kuhusiano wenu uweze kudumu.

3.Kuwa unampenda mtu mwingine mahali

KIla siku lazima tupatane na watu tofauti, na kuwapenda zaidi kuliko wapenzi wetu lakini husimwambie mpenzi wako kwa maana ataona umemdharau lakini jaribu uezalo kumpenda mpenzi wako.

 

4.Unamfuatilia aliyekuwa mpenzi wake kisiri

Endapo tumepatana ndio nilikuwa katika uhusiano wa kimapenzi na kisha tukaachana lakini kuna wae wanatabia ya kufuatili wapenzi hao, ndio lazima ufahamishwe zaidi lakini kama umekuwa ukifuatilia aliyekuwa mpenzi wake.

5.Kuwa umekuwa ukifuatilia maisha yake na kuchunguza mambo yake

Kama ni kuchunguza haya basi usimfahamishe mpenzi wako kuwa unafuatilia maisha yake au umekuwa ukimchunguza.