Ndio hawa maceleb wanawake ambao wanafanya kazi hata baada ya kupeana na kupewa talaka

Muhtasari
  • Wanawake ambao wanafanya kazi hata baada ya talaka
Lilian muli
Lilian muli

Ukipewa talaka na mume wako au mwanamke akipea mumewe talaka hilo halimaanishi kuwa utakaa kwa nyuumba na kulia miaka yako yote.

Kumbuka kuwa una watoto ambao wanahitaji ujasiri wako na wanakuhitaji hasa wakati huo wa kipindi hicho kigumu.

Kuna wanawake maceleb ambao wamethibitisha kuwa kupewa au kupeana talaka si mwisho wa dunia mbali wapaswa kuendela na maisha yako kama kawaida na kutunza watoto wako.

Hii hapa orodha ya wanawake maceleb ambao wanafanya kazi licha ya kuwa wametengana na waume zao;

1.Betty Kyallo

Baada ya harusi yao ya kifahari na ya kipekee, miezi sita baadae mwanabiashara na aliyekuwa mwanahabri wa runnga ya K24 Betty na mwanahabari Dennis Okari walipeana talaka.

Wawili hao wamebarikiwa na mtoto mmoja wa msichana, Betty ni mfano mwema ya kwamba talaka si mwisho wa maisha au dunia kwa maana kila siku mwanabiashara huyo anafanya mambo mapya ya kuendeleza maisha yake.

2.Lilian Muli

Mwanahabari huyo wa runinga ya Citizen Muli alimpea Kanene talaka baada ya mambo mawili au matatu huku akijutia kuwa katika uhusiano mbaya katika maisha yake.

Lilian sasa ni mama wa watoto wawili.

2.Akothee

Ni msanii ambaye anafahamika sana humu nchini na hata nje za nchi huku, akimpa mumewe wa kwanza talaka na kuendelea na maisha yake.

Akothee amekuwa akitia bidii katika kazi yake ili kuwalea wanawe watano.

3.Anne Kiguta 

Ni mwanahabari wa runinga ya K24, aliachana na mume huku mtoto wao akiwa na miaka mitatu hii ni baada mumewe kuleta vurugu katika ndoa yao.

4.Terryanne Kibet

Aliamua kuwa talaka si jambo kubwa kwake huku akiendela na maisha yake  na kuwalea watoto wake