Mimi nikifa uniposti nitakutokea usiku, kaa na unifiki wako-Nyota Ndogo awaambia wanafiki

Muhtasari
  • Nikifa wengi watakuwa kwenye mitandao ya kijamii wakinisifia na nikiwa hai hawanisifu
  • Ukinipoati nikifa nitakutokea usiku, Nyota ndogo awaonya wanafiki
83532576_627204834703118_8454513908795708531_n
83532576_627204834703118_8454513908795708531_n

Msanii anaye pendwa sana na mashabiki wake Nyota Ndogo,kupitia kwenye mitandao yake ya kijamii ya instagram ameposti ujumbe wa jinsi wanafiki watakavyo msifu na kujifanya kuunga mkono usanii wake ilhali akiwa hai wanajifanya.

Msanii huyo kupitia kwenye ujumbe wake wa kuchekesha alisema kwamba watu wengi watakuwa mitandaoni huku wakimsifu jinsi alikuwa msanii mwenye talanta ilhali akiwa hai hawamuungi mkono wala kumsifia.

"Ngoja nawape picha mtakazo zitumia kuandika R.I.P nitakapo ondoka dunia najua zitakua nyingi mpaka Wasio post ama kusapoti mziki wangu pia wakiskia wataandika maskini alikua mwanamziki Mzuri nakumbuka nyimbo yake moja bla bla bla." Aliandika Nyota Ndogo.

Msanii huyo wa kutoka katika mkoa wa pwani alisema kuwa waliokuwa wanafiki heri wakae na unafiki wao kwa maana endapo siku hiyo watamposti wakimsifia haya basi atawatokea usiku huo licha ya yake kuwa ameaga dunia.

"Wewe ukinipost nikifa nitakutokea usiku bora ukae na unafiki wako."

nyota.
nyota.

Nyota alikuwa anawaambia mashabiki wake kuwa video ya kibao chake kipya 'Woman' tayari iko kwente youtube.

Ni kibao ambacho amemshirikisha mumewe.