Uzani

Anerlisa apunguza uzani baada ya kubwaga kilo 14 ili kutoshana na marehemu dadake Tecra

Anerlisa amepunguza kilo 14

Muhtasari

 

 Anerlisa ameichukua hatua hiyo ili kuziweka hai kumbukumbu za dadake 

 

Anerlisa Muigai amekuwa akiwaonyesha mashabiki wake kuhusu anavyopiga hatua nzuri katika kupunguza uzani .

  Amefichua jinsi alivyofaulu kubwaga kilo 14  kwa ajili ya kujitolea na bidii ya kuafikia lengo lake ili kutoshana kama alivyokuwa dadake Tecra .

 

Tecra  aliaga dunia baada ya kuanguka na kupata majeraha mabaya kichwani  Aprili tarehe 27 mwaka huu alipokuwa na mpenzi wake Lali Omar huko Lamu .

Lali  mwenye umri wa miaka 54, alishtumiwa kwa kusababisha kifo chake na hata akafikishwa kortini . Alizikwa nyumbani kwao Naivasha mei tarehe 16 na kama hatua ya kuhaisha kumbukumbu zake ,dadake  Anerlia ameamua kupunguza uzani ili atoshane na dadake