Aina ya wanaume wanawake wanapaswa kuepuka ikiwa hawataki maisha duni

Muhtasari
  • Aina ya wanaume wanawake wanapaswa kuepuka ikiwa hawataki maisha duni

Wanaume wengi kabla ya kuoa au kuwa katika uhusiano lazima ajigambe kiasi ili mwanamke amuone kuwa anaweza katika maisha.

Kuna wanawake ambao huoenda mwanamume kwa ajili ya pesa, sura na kusahau kuwa tabia ni kitu muhimu cha kuangalia katika mwanamume.

Wengi wameingia katika ndoa lakini wanaachana baada ya muda mfupi  kwa maana hawakuchagua vyema, wengi walichaguliwa na wazazi na wengine walichagua kwa haraka kwa maana waliona muda umewapita na wamechelewa.

 

Kuna aina ya wanaume ambao wanawake wanapswa kuepukana nao kama hawataki maisha duni au maisha ya kilio kila siku.

Baadhi ya aina ya wanaume hao ni kama vile wafuatao;

1.Mwenye sura nzuri lakini ana kiburi

Wanaume kama hao hawana chochote wacha tu majivuno ya sura yao, baadhi yao huwa wanajigamba na vitu vya wenyewe na kudai ni vyao.

Kama mwanamke hayuko makini atamuoa na kuenda kuona mateso ambayo hakutarajia.

2.Mwanamume ambaye anapenda mali yake

Ndio hatukatai wanaume wanapaswa kupenda mali ambayo wametafuta na jasho lao, lakini kuna wale upendo wao wameweka kwa mali tu na wala hafikirii kitu kingine kile.

 

Mkiongea jambo moja au lingine lazima ataje utajiri na mali yake.

3.Mwanamume ambaye ni mbinafsi

Kila kitu anajifanyia tu yeye ukimwambia akusaidie na jambo au kiwango cha pesa fulani kwanza anajisaidia  haya basi kama mwanamke fahamu kuwa mwanamume kama huyo hawezi kukusaidia maishani mwako.

4.Mwanamume ambaye hana maono ya siku zijazo

Wanaume kama hao huwa wanakaa mahala pamoja bila ya kujiendeleza wala kufikiria siu za usoni na hata kupanga jinsi ataanzisha maisha yake na kuwa na majukumu kama baba mwenye familia

Karne hii ya sasa vijana wengi hawana maono ya siku zijazo wanataka tu kukaa na wazazi wao hili wasijukumike.

5.Mwanamume ambaye anapenda vileo

Wanaume kama hao hupeleka pesa zao kubugia vileo na kutojiendeleza maishani huku wakiwapa wanawake kazi ngumu ya kuwalea watoto.

Wanawake wanapaswa kuepuka mwanamume kama huyo kama hataki kuishi maisha duni katika siku zake za usoni.