'Hatuko kwa mashindano,'Churchill asema huku akikana madai haya

Muhtasari
  • Mcheshi Mwalimu Churchill akana madai kwamba anabishana na wasanii wenzake ili kupata umaarufu
  • Churchill alikuwa anampongez aEric Omondi kwa kuzindua studio yake hivi majuzi
Mwalimu churchill
Image: Hisani

Mfalme wa ucheshi Daniel Ndambuki almaarufu Mwalimu Churchill amekanusha madai ya kwamba anabishana na wasanii wenzake ambao wamekulia katika mikono yake ili kupata umaarufu zaidi.

Hii ni baada ya mchekeshaji Eric Omondi kuzindua studio yake hivi majuzi huku Churchill akimpongeza na kusema kwamba hayuko kwenye mashindano.

Pia alikuwa anamjibu shabiki mmoja ambaye aliandika ujumbe huu;

"Ni vema kumsherehekea mtu anaponawiri kwa jambo lolote lile haswa mshindani wako, hebu na tufurahie maisha ya kila mtu."Shabiki huyo aliandika.

Akijibu ujumbe huo, Churchill alisema kwamba habishani na msanii yeyote ila anafurahia jinsi wanavyonawiri kwenye kazi zao za usanii.

" Hatuko kwa mashindano yeyote ila nafurahia sana nikiona wasanii wakifanikiwa kupitia mikononi mwangu." Churchill alisema.

Madai yake yanajiri siku chache baada ya shabiki mmoja kumuuliza huwa anawalipa wacheshi pesa ngapi, kwa werevu wake Churchill alimuuliza kama ana pesa nyingi ambazo anataka kuwalipa.