'Nilikuwa na shida ya septamu iliyosababisha kuharibika kwa mimba-Jacque Maribe

Muhtasari
  • Jacque Maribe ameeleza jinsi alipigana na shida ya tumbo la uzazi huku akisema kwamba aliharibikiwa na mimba mara mbili
Jacque Maribe
Jacque Maribe

Kwa mara ya kwanza aliyekuwa mwanahabari wa runinga ya Citizen Jacque Maribe amefichua kuwa aliharibikiwa na mimba mara mbili kabla ya kumzaa mwanawe.

Akiwa kwenye mahojiano alieleza jinsi alipigana na suala la uzazi.

"Nilikuwa karibu kupata mtoto awali lakini mimba yangu iliharibika, ni jambo ambalo lilikuwa ngumu kwa maana lilikuwa jipya kwangu.

 
 

nilijaribu tena kubeba mimba lakini ikashindikana na sikujua ni nini ilikuwa inaendelea, daktari waliamua kufanya uchunguzi zaidi na kupata na shida na septamu

yangu ilikuwa na ukuta katikati na tukagundua kuwa shida ilikuwa mtoto alikuwa upande mmoja endapo kuta hizo zinakua mtoto hakui na kusababisha kuharibika kwa mimba." Alieleza Jacque.

Septamu ni hali ya kugawanya tumbo la uzazi mara mbili wakati wa ukuaji wa mtoto katika tumbo la uzazi.

HUku akieleza nini haswa kilitendeka alisema kwamba alikuwa afanyiwe upasuaji ili kutoa shida hiyo kwenye tumbo la uzazi lakini kwa bahati nzuri akampata Zahari.

Alisema kwamba baada ya upasuaji huo walikuwa wameambiwa wajipe muda.