...Simu zangu haushikangi,'Huu hapa ujumbe Akothee aliomwandikia mtangazaji Maina Kageni

Muhtasari
  • Msanii Akothee amemshukuru mtangazaji Maina wa Kageni kwa kumuamini licha ya yake kutofahamu hayo
AKOTHE
AKOTHE

Kwa mara ya kwanza msanii Akothee aliweka wazi kwamba mtangazaji Maina Kageni amekuwa akimsaidia sana katika kazi yae.

Kupitia kwenye ujumbe aliouandika katika ukurasa wake wa instagram Akothee alidai kwamba amegundua kuwa mtangazaji huyo amemuamini katika kazi yake.

"Wacha nichukue fursa hii kumshukuru mwanamume @mainakageni kwa kuniamini maina sifa zako nimezipata kwa sanaaa kampuni zikimuuliza nani atawafanyia kazi ya kuuza bidhaa zao vyema hivi ndivyo Maina husema

MAINA WA KAGENI : Ayiyiyiyiiiyi, Haki chukua AKOTHEE HAKI hautaregret, Huyo Dem Ni mnoma kwa brand visibility. atakufanya upende bidhaa zako sana." Ujumbe ulisoma.

Alifichua kuwa kwa sasa amepokea kazi tano kwa ajili ya Maina, na hawezi chukulia msaada huo kwa mzaha.

"Maina nimepokea majibu matano kutoka kwa kampuni tofauti kwa ajili yako,japo kuwa sikujua kwamba unaniamini, unanipa msaada sana hivyo na hata haunipigiangi simu kunichocha bike unaniuza, na hata simu zangu haushikangi 😂😂😂😂

Maina wa Kageni MUngu akubariki saaana." Aliandika Akothee.