'Tuliachana na Jowie kabla aende jela,'Jacque Maribe akanusha madai waliachana na Jowie akiwa jela

Muhtasari
  • Jacque maribe akana madai kuwa waliachana na Jowie akiwa jela
  • Hii ni baada ya Jowie akiwa katika mahojiano na radiojambo kusema waliachana akiwa jela
  • Maribe alisema wakati wa kesi hiyo kila kiyu kilisimama mpaka kazi yake ilikuwa kama kutazama sinema mbaya
maribe
maribe

Baada ya Jacque Maribe kufahamika sana mwaka wa 2018, alipotea kwenye vyombo vya habari baada ya kuhusishwa na mauaji ya mwanabiashara Monica Kimani.

Aliyekuwa mpenzi wake Jowie Irungu alikuwa mshukiwa mkuu katika kesi hiyo.

Wawili hao waliweza kutoka korokoroni baada ya muda huku wakiwa kwenye vichwa vya habari kwa muda.

 

Akiwa kwenye mahojiano Jacque alikanusha madai kwamba waliachana na Jowie alipokuwa jela.

Awali Jowie akiwa kwenye mahjiano na radiojambo alisema kwamba waliavhana alipokuwa jela.

"Tulipatana nilipokuwa kazini, baadhi ya marafiki zangu walijua kuwa tulikuwa tumechumbiana, alikuwa mtu mzuri sana sitawahi jiyokeza siku moja na kusema jambo kinyume chake

alikuwa mzuri kwangu, nafikiri kwamba ni muhimu kusoma mtu kabla ya kukimbilia mambo kama haya naamini tuliharakisha mambo." Alisema Jacque.

Mama huyo wa mtoto mmoja alisema kwamba hapendi kuzungumzia Jowie kwa maana watu watamhukumu akisema ukweli wake na kusea kwamba bado ana uchungu.

"Nataka kukosoa alichosema kwamba tuliachana alipokuwa jela wavha tuwe waaminifu, tuliachana kabla ya kukamatwa lakini si mtu ambaye ningependa kudada tayari hii ni habari tutafanya baada ya kesi kukamilika

Nadhani ni muhimu watu kufahamu ukweli kutoka kwa waathiriwa wenyewe." Alisema Jacque.