Mpenzi wangu alinitema siku ya kusheherekea mwaka mpya-DR Ofweneke afichua haya

Muhtasari
  • Mchekeshaji Ofweneke aeleza jinsi aliachwa na mpenzi wake wakati wa kusheherekea mwaka mpya
  • Pia alieleza jinsi alivyopigana na maumivu ya moyo baada ya kuachana na Nicah
Dr-Ofweneke
Dr-Ofweneke

Mchekeshaji DR Ofweneke alifichua kuwa kuna siku alitemwa na mpenzi wake siku ya kusheherekea mwaka mpya huku akimwambia hawezi vumilia maisha yake na kutegemea malipo ya ucheshi wake.

Miaka,14 baadae mcheshi huyo bado anakumbuka jinsi alitemwa na mpenzi wake.

Akiwa kwenye mahojiano alikuwa na haya ya kusema;

 

"Nilitemwa siku kusheherekea mwaka mpya, huyu mwanamke alikuja na kuniambia hafikirii kwamba ucheshi wangu utanipeleka mahali

Na hajui kama nitakuja kufaulu kwa vyovyote na hawezi vumilia, nilikuwa nimefanya ucheshi wangu wa kwanza na kulipwa shillingi 200, nilimnunulia bangili aliniuliza hii ni nini mimi ni modella." Alielza Ofweneke.

Mcheshi huyo alisema kuachana na mpenzi wake Nicah kulikuwa uchungu sana kwa maana walikuwa na watoto pamoja.

Alisema kwamba ulikuwa uamuzi mgumu kwa maana alikuwa anachagua furaha ya wanawe na furaha yake mwenyewe.

Baada ya kuachana na Nicah alisema kwamba alitafuta nyumba na kuanza maisha yake ambapo alikuwa analia sana.

"Wakati ambao nilikuja kupona, nilikuwa nimeumiza wanawake wengi sana ambao sikujali kuwahusu."