Jinsi ya kuishi maisha yako wakati unasubiri upate mpenzi wako wa maisha

Muhtasari
  • Jinsi ya kuishi maisha yako wakati unasubiri upate mpenzi wako wa maisha

Si wanaume au wanawake wote ambao wamebarikiwa au kubahatika kuwa katika uhusiano wa kimapenzi.

Kuna wale wanasubiria Mola awabariki na wapenzi na wengine wamejipa mapumziko baada ya kuumizwa mioyo yao na kuamua wanahitaji sasa mpenzi wa maisha na wala si wa muda mfupi.

Kuna vile mwanamume au mwanamke anapaswa kuishi maisha yake huku akimsubiri mpenzi wa maisha yake.

 

Na hizi hapa njia za kuishi endapo unamsubiri mpenzi wako;

1.Jifunze mambo mapya

Kam wataka uhusiano wako ambao unatarajia kuwa nao haya basi jifunze mambo mapya na wala usilete mambo ya uhusiano huo mwingine katika uhusiano wako wa kimapenzi wa sasa.

2.Wakati mwingi na familia

Kwa maana wakati huu hujashikana na mtu yeyote tenga muda wako ili ukae na familia yako, ndiposa ukipata mpenzi usiharibu muda wako mwingi kwa familia badala utumie muda wako naye.

3.Jijue na ujifahamu

Kuna wanawake na wanaume ambao hawajijui  wao ni akina nani na wanataka nini maishani, kwa maana wakati huu una muda haya basi jisome na ujifahamu wewe ni nani.

 

4.Ongeza ujuzi wa mawasiliano

Kama uhusiano hio mwingine mliachana kwa ajili ya kuto wasiliana, wakati huu ambao unasubiria kupata mpenzi wako ongeza ujuzi wako ili kusiwe na taabu yeyote.