Sababu ambazo hufanya bwana harusi kulia wakati wa harusi

Muhtasari
  • Sababu ambazo hufanya bwana harusi kulia wakati wa harusi

Wakati mwingine tumewaona bwana harusi wakitokwa na machozi wakati bi Harusi anatembea kuenda kwenye madhabau ili waweze kuunganishwa na kuanza maisha ya ndoa pamoja.

Kwa kawaida kila mtu ambaye amehudhuria harusi hiyo huwa shahidi ya harusi hiyo.

Lakini kuna wale ambao huwa wanajiuliza haswa kwanini bwana harusi hulia  wakati huo, hizi hapa baadhi ya sababu kwa nini bwana harusi hutiririkwa na machozi wakayi huo maalum;

1.Mtoto wa mama

Wanaume wengi karne hii ya sasa wanawapenda akina mama zao huku wakikumbuka sasa hatakuwa akimpa mama usaidizi wote ambao anataka kwa maana sasa ameongezewa majukumu mengine.

2.Kujionyesha tu

Ndio kuna wale ambao hutiririkwa na machozi wakikumbuka yale wamepitia kama wapenzi na kumshukuru Mungu kwa maana muda umefika wa kupokea mpenzi wake bila pingamizi yeyote.

Lakini kuna wale wanataka watu watie umakini wao kwake na kuonyesha kuwa anampenda mpenzi wake.

3.Akikumbuka mahaba yao

Wengi ukumbuka kumbukumbu za mahaba ya mapenzi yao na kudondokwa na machozi na kutoamini au mida umewadia mpenzi wake awe wake w maisha.

4.Kujawa na hisia

Wanaume wengi hujawa na hisia endapo kumuona mpenzi wake anaingia kanisani na nguo yake ya harusi na kushindwa kushikilia machozi yake kwa ajili ya furaha.