Ni msanii yupi kati ya hawa anastahili tuzo mwaka huu?

Muhtasari
  • Ni msanii yupi kati ya hawa anastahili kutuzwa mwaka huu wa 2020
Mejja
Image: Hisani

Kwa hakika wasanii wengi humu nchini hasa wakati huu wa janga la corona wamejikakamua na kutoa wimbo baada ya wimbo ili kuwaburudisha mashabiki wao.

Kuna wale baada ya baadhi ya mambo kupigwa marufuku walilegea katika kazi yao ilhali kunawale walitia bidii katika kazi yao bila ya hata kulaza damu.

Lakini kwa maoni yako ni msanii yupi kati ya hawa anastahili tuzi mwaka huu wa 2020?

1.Sauti sol

Bendi ya Sauti Sol ni moja wapo wa bendi ambayo imeonyesha ushirikiano na kutia bidii katika kazi yao licha ya changamoto ambazo kila mmoja hupitia.

Bendi hiyo ilianza usanii wao mwaka wa 2005, huku wakati wa corona wakitoa albamu yao mpya inayofahamika kama 'Mid night train'.

2.Mejja

Mejja Meme Hadhija alianza kazi yake ya usanii akiwa katika shule ya msingi huku akifahamika sana kwa ajili ya kibao chake cha 'Landlord'

Wakati huu wa janga hili Mejja ameshirikiana na wasanii wenzake na kufanya collabo ambazo zimevuma sana na kupendwa na mashabiki.

3.Otile Brown

Otile ni msanii ambaye amekuwa katika usanii zaidi ya miaka mitano, huku mwaka huu akiachili albamu yake ya 'Just In love'

4.Nadia Mukami

Safari ya muziki ya Nadia inafahamika na wengi uku akitoa vibao vyake wakati huu wa corona na kupendwa sana na mashabiki.

Kibao chake huku akimshirikisha Sanaipei cha 'Wangu' kilipendwa na mashabiki huku kikipokea watazamaji wengi kwenye youtube.

5.Khaligraph Jones

Msanii huyo alianza kuimba mwaka wa 2004, huku akitia bidii katika kazi yake na kuanza kutoa kibao kimoja baada ya kingine.

Mwezi jana msanii huyo alitoa wimbo unafahamika kama 'Kwenda'.