'Wacha kucheza na watumishi wa Mungu',Msanii Ringtone amuonya msanii Willy paul

Muhtasari
  • Ringtone amuonya Willy Paul kwa mara ya mwisho kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram
  • Msanii huyo alimwambia pia kuwa awache kucheza na watumishi wa Mungu
ringtone
ringtone

Vita kati ya msanii Ringtone Apoko na Willy Paul zimeshuhudiwa kwa muda kwenye mitandao ya kijamii.

Wawili hao wamekuwa wakipeana vita vya maneno huku, kupitia kwenye ukurasa wake Ringtone akimpa msanii huyo onyo.

Kupitia kwenye video ambayo alipakia kwenye ukurasa wake wa instagram alimwambia kwamba awache kucheza na watumishi wa Mungu kwa maana kuna nguvu katika jina lake yesu.

 

"Willy Paul nataka kukuongelesha leo uliwacha tasnia ya muziki wa injili kwa maana hukungoja nguvu zake roho mtakatifu

Ni kijna ambaye ni wakamati wa roho chafu, wacha kucheza nasi watumishi wa Mungu naweza kukuombea saa hizi pesa ikupotee na ukonde, ata nikuombee wanawake ambao unawadanganya watoroke

Willy Paul wacha kucheza na watumishi wa Mungu, nawea kukuombea break yako ya nyuma ipotee huwe unahara pilipili, naeza kukuombea uwe huna chochote, tubanye shetani au tukubanye 

Nakuonya kwa mara ya mwisho." Aliongea Ringtone.