Watu mashuhuri walio jifungua mwaka 2020

Muhtasari
  • Orodha ya watu mashuhuri waliyojifungua mwaka wa 2020
Corazon-Kwamboka-pregnant-696x418
Corazon-Kwamboka-pregnant-696x418

Wengi walitangaza habari za ujauzito wao kupitia mitandao ya kijamii, na hata kubarikiwa na watoto.

Hii hapa orodha ya watu ambao wamejifungua mwaka wa 2020 licha ya kuwepo kwa janga la corona.

1.Grace Msalame

 

Msalame alijifungua mwezi Oktoba huku akibarikiwa na mtoto wa kiume, alitangaza habari hizo kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram.

2.Corazon Kwamboka

Huku akizungumzia kujifungua kwake Corazon alisema kwamba ni uchungu kwa sababu ilikuwa mara yake ya kwanza.

Corazon alijifungua Agosti mwaka huu.

3.Lady Mandy

Ni mkewe msanii wa bendi ya Sauti sol Polycarp na alijifungua Agosti 26 mwaka huu.

4.Saumu Mbuvi

 
 

Mwanawe aliyekuwa gavana wa kaunti ya Nairobi Mike Sonko, alijifungua mtoto wake wapili mapema mwaka huu, mwezi wa Machi.

5.Jacqy Tina

Muigizaji wa kipindi cha mother-in-law alijifungua mwaka huu.

(MHARIRI: DAVIS OJIAMBO).