'Hatukujua kuwa mama yangu alikuwa na uvimbe,'Mejja asimulia haya

Muhtasari
  • Hatukujua kuwa mama yangu alikuwa na uvimbe kwa maana hatukuwa na pesa msanii Mejja asimulia maisha yake ya utotoni
Mejja
Image: Hisani

Msanii Mejja akiwa kwenye mahojiano alisimulia changamoto alizopatana nazo alipokuwa anakua.

KUna baadhi ya wasanii na watu mashuhuri ambao wana hadithi za kukuguza moyo na kuwatia wanamitandao mioyo na kuwafanya wasikate tamaa.

"Tulipokuwa katika shule ya msingi tulikuwa na maisha mazuri kwa sababu nyanya yangu alikuwa na pesa

 

Baada ya yake kuaga dunia tulifahamishwa kwamba mama yangu si mtoto wa nyanya yangu,jamaa zetu walikataa mama yangu kurithi mali yeyote ya nyanya yangu 

Kufanya mambo mabaya zaidi mama yangu alikuwa anaumwa na kichwa kila wakati hayukujua kwamba alikuwa na uvimbe kwa maana hatukuwa na pesa kuenda kwa mtalaamu." Alisema Mejja.

Mejja alianza kufanya kazi tofauti ili kujikimu kimaisha na kupata riziki yake, huku akivutiwa kuwa mwanamziki baada ya kumtazana ndugu yake akiimba

"Nilifanya kazi nyngi ata kuuza njugu, mwanamme mmoja alinipa kazi ya kuosha hoteli yake na kunilipa chakula cha mchana

Nilivutiwa na usanii nilipomuona ndugu yangu akiimba,nilianza kuiga uimbaji wake, nanikaanza kuandika nyimbo wakati huo nilikuwa nauza mogoka."