'Nitakupenda milele,'Msanii Benpol amtakia Anerlisa Muigai siku njema ya kuzaliwa huku akijibu

Muhtasari
  • Benpol amtakiaAnerlisa heri njema ya kuzaliwa kwa ujumbe wenye maneno ya mahaba kweli kweli
gVUk9kpTURBXy80NTA3YjEwNDQxOGFhMDQ1MTFlOGFiZDU2NDk5MDJiZC5qcGeSlQLNAxQAwsOVAgDNAvjCw4GhMAE
gVUk9kpTURBXy80NTA3YjEwNDQxOGFhMDQ1MTFlOGFiZDU2NDk5MDJiZC5qcGeSlQLNAxQAwsOVAgDNAvjCw4GhMAE

Msanii Benpol mumewe Anerlisa Muigai kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amemtakia mkewe siku njema huku akisheherekea siku yake ya kuzaliwa.

Benpol alisema kwamba hana mengi ya kusema siku hii maalum ya mkewe bali ataona kupitia kwa matendo yake.

Anerlisa amefikisha miaka 33, huku wanamitandao wakisema kwamba bado yeye ni mchanga.

 

Pia mumewe Anerlisa alimshukuru kwa kuwa mkewe kwa kumuamini, huu hapa ujube wake Benpol.

"Heri ya kuzaliwa mke wangu mzuri, mwamba wangu. kila kitu changu nakupenda kutoka moyoni mwangu na nitakupenda milele

Sina maneno mengi ya kusema lakini vitendo utaviona 🙏🏾. asante sana kwa kuweka matumaini yako kwetu wacha Mungu akakubariki kila wakati hadi miaka mingi zaidi, mafanikio na afya njema." Aliandika Benpol.

Huku Anerlisa akisheherekea siku yake ya kuzaliwa mashabiki, marafiki walimtakia heri njema.

Huku akimjibu mumewe Anerlisa alimshukuru pia mumewe kwa ujumbe wake mwema huku akimwambia amuweke Mungu mbele katika ndoa yao.

"Asante sana mume wangu kwa maneno yako yenye upendo, nitakushukuru kila siku na kukupenda milele

Wacha tueke Mungu mbele wewe ni wa ajabu Benard. MUngu akubariki kila mara." Alijibu Anerlisa.