Ndio hawa!wakenya mashuhuri waliyooa mashabiki wao

Muhtasari
  • Kutana na wakenya mashuhuri waliowaoa mmoja wa mashabiki wao

KIla mtu ana msanii, muigizaji,mtangazaji,mchekeshaji,mwanahabari ambaye anampenda na kuwa shabiki wake sugu.

Ni upendo ambao ata akipata kejeli kutoka kwa wanamitandao utamtetea kwa vyovyote vile.

Kuna baadi ya wakenya mashuhuri ambao walioa mmoja wa mashabiki wao na hii hapa orodha yao.

 

1. Rashid Abdalla na Lulu Hassan

Wawili hao walipatana mjini Mombasa amba[o Rashis alikuwa nafanya kazi katika kituo kimoja cha redio.

Lulu alikuwa shabiki wake, huku wawili hao wakifunga pingu za maisha na kuwa wanahabari.

lulu 2
lulu 2

Baada ya muda wawili hao walianza kufanya kazi katika runinga ya Citizen.

2.Bahati na Diana Marua

Diana alikuwa shabiki sugu wa nyimbo za Bahati, baada ya muda wawili hao waliweza kuona na kubarikiwa na watoto wawili.

bahati1__1570190817_94158
bahati1__1570190817_94158

Awali wamekuwa kwenye vichwa vya habari kwa mambo tofauti, licha ya kejeli ambazo hupokea wameonyesha mahasidi kwamba upendo wao ni wa milele.

 

3.Njugush na Celestine Ndinda 

NJugush anafahamika kwa ucheshi wake na uigizaji wake wa kipekee, kupitia kwa kaiz yake Ndinda alikuwa shabiki wake huku akimkubali na kumuoa.

njugu
njugu

4. Msanii Wyre 

Msanii huyo anafahamika nchini kwa mtindo wake wa uimbaji, mkewe alikuwa shabiki wake huku wakifunga pingu za maisha kwa harusi ya kipekee.

Wyre
Wyre

5.Willis Raburu na Mary Prude

Wawili hao walifunga pingu za maisha na kisha mwaka jana waachana baada ya kumpoteza kifungua mimba wao.

Mary alikuwa shabikiye Raburu.

willis raburu and wife marya
willis raburu and wife marya

Miongoni mwa wakenya wengi mashuhuri ni pamoja na rappa Octopizzo ambaye alimuoa shabiki wa nyimbo zake.