Mpango wangu wa kando alinichapa na kuniumiza baada ya kutopokea simu yake-Mwanamke Asimulia

Muhtasari
  • Mwanamke asimulia jinsi alivyochapwa na mpango wake wa kando baada ya kutopokea simu yake
black-woman-crying-
black-woman-crying-

Ni jambo ambalo limechukuliwa kuwa la kawaida humu nchini , baada ya wasichana wadogo kuwa na 'Sponsor' na hata vijana kuwa na 'sigar mummies'.

Lakini cha kushangaza ni vile wana ndoa wanakiri kuwa wamekuwa na mipango wa kando kwa miaka ilhali bibi au waume zao hawajui wala kufahamu hayo.

Je ina maana kuwa watu wameacha kuchukulia ndoa kama jambo la maana na la kupewa heshima?

 

Mwanamke mmoja aliwaacha wasikilizaji wa radiojambo midomo wazi baada ya kufichua kichapo ambacho alipokea kutoka kwa mpango wake wa kando baada ya kutopokea simu yake.

"Mimi nilikuwa na mpango wa kando, ambaye tulikuwa tumekaa naye kwa muda wa miaka mitano

Siku moja nilienda kwenye mkutano, nilipata akiwa amenipigia simu lakini singepokea kwa maana nilikuwa kwenye mkutano

Niliporudi kwa nyumba nilimpata akiwa amekasirika sana, alinichapa na kuniacha na majeraha ambayo hadi leo huwa namkumbuka nayo

Alikuwa anadai kwamba nilikuwa kwa mwanamume mwingine ilhali ilikuwa ni uongo,tangu hiyo siku tuliachana

Ndio alikuwa na familia na watoto, lakini sikuwa nimeolewa." Mwanamke Huyo Alisimulia.

Sio wanawake tu pekee ambao wanajua kufichua siri za maisha yao, mwanamume mmoja alisema kwamba alikuwa na mpango wa kando ambaye alisababisha bibi yake kuondoka na kumuacha.

 

"Nilikuwa na mpango wa kando, ambaye alifana bibi yangu atoke kwa ndoa, baada ya kutoka nilimuoa lkini hatukukaa kwa muda mrefu akaenda pia."

Je mpango wa kando hawapendi majukumu au wanataka kuishi maisha yao pekeyao?