Sababu kwa nini wabunge wengi ni maskini licha yao kupokea kiasi kikubwa cha mishahara na posho

Muhtasari
  • Sababu kwanini wabunge wengi ni maskini licha yao kupokea kiasi kikubwa cha mishahara na posho

Wananchi wameishi kujiuliza kwanini hali ya wabunge wengi wa humu nchini ni ya umaskini licha ya wao kupokea kiasi kikubwa cha mishahara na posho.

Swali ambalo pia wanapaswa kujilaumu kwa njia moja au nyingine.

Lakini sababu ni ipi ya wabunge kuwa maskini licha ya wao kuitwa waheshimiwa na kupewa heshima kubwa na wanachi?

 

Hizi hapa baadhi ya sababu ya maswali ya wananchi wengi;

1.Rehani za mikopo na ushuru

Utawapata wabunge wengi wamo na madeni tofauti katika maisha yao, huku waking'ang'ana kulipa mikopo ambayo wamechukuwa kwenye benki.

Ndio wengi watang'ang'ana kulipa ili kudumisha jina la mheshimwa na wala wasipatwe na aibu mbele ya wananchi, bila ya kujua maisha yao ya kesho wala kuekeza pesa za maisha ya usoni.

2.Hawana wakati wa kukimbia

Kama mfanyakazi uwezi tegemea mshahara tu pekee bali wapaswa kuweka ata kama ni biashara ili kupata mapato mengine ya maisha.

Lakizi utapata wabunge wengi hawana wakati wa kuweka biashara wla kuchunguza ni biashara ipi ataweza kufanya.

 

Kazi ya kuandika si ya milele kuna wakati utafika na kazi yako itakwisha lakini swali kuu ni ukifutwa kazi utatagemea nani?

3.Kuto pesa kwa Harambee na mazishi

Ata kama si kila siku kila wikendi utawapata wabunge wamealikwa kwenye harambee na kwa sababu wanataka kushinda kuitwa mheshimiwa atapeana pesa nyingi bila ya kufikiria maisha yake.

Yaani kwa ufupi tuseme wanatambua jina la mheshimiwa sna kuliko maisha yao.

Mbunge asipotoa au itika wito wa wananchi wengi watasema kya kwamba ni mchoyo na anajipenda.

Akifilisika wananchi watabaki na maswali kwanini mbunge fulani ni maskini.

Kama wananchi pia tunapaswa kufahamu ya kwamba tumechangia wabunge wetu wawe maskini kwa kuwategemea.