'Utapata bwana kweli,'Mashabiki washambulia msanii Zuchu baada ya kupakia picha hii

Zuchu-cover-for-her-new-song
Zuchu-cover-for-her-new-song

Msanii Zuchu ambaye amesajiliwa na lebo ya WCB amabayo imemilikiwa na staa wa bongo Diamond Platnumz amekuwa akipakia picha kwenye ukurasa wake wa instagram.

Zuchu alipakia picha akiwa amevalia fulana huku mashabiki wakimkejeli kwa ajili ya mavazi yake.

Msanii huyo ameshikwa mkono na Diamond katika safari yake ya usanii, ni watu wachache ambao wanaweza kukushika mkono katika safari yako hadi waone mafanikio yako.

 
 
 

Diamond amemuinua Zuchu kwa njia moja au nyingine, huku madai yakiibuka kwamba Zuchu ndiye alikuwa chanzo cha Diamond kuachana na Tansha Donna huku baadaye Zuchu akikana madai hayo.

Zuchu hakumaliza mwaka mmoja bali alivuma kwenye mitandao kwa ajili ya nyimbo zake zilizopendwa na mashabiki baada ya kusajiliwa na WCB.

Haya basi sifa kando, mimi na wewe tunafahamu vyema mitaa ya mitandao ya kijamii lazima upendwe na wakati mwingine ukejeliwe na mashabiki kwa yale ambayo wameona ni mabaya kwao.

Haya basi Zuchu alipatana na upande mbaya katika mitaa ya mitandao ya kijamii baada ya kupakia picha huku akiwa amevalia fulani.

Tuweze kusoma na kutazama hisia za wanamitandao;

adabethchilla: Ndio mavazi aliyo vaa kama hana wazazi ety mtoto wa marekan labda kweli hata mavazi yanamtambulisha kuwa no mmarekani

 

officialzeusoo:Jamani Umevaa sweater au nini hiyo

 

deemiroe20: dada anguu nguo kama Hii Utapata bwana Kweli?

fadhilnajiath:kumbuka wewe ni mtoto wa kiislam

nurdinnjumbe58: Dah Ila huyu mtoto saa nyengine

jailos_music_studio: Zuchuuuu umevaa Aul limekuvaa

adestoezekia: Duh we Zuchu vazi gani hilo

aziza.kapela.54: Na hy misweta yako sasa yan wewe unavinguo vya ajabu ajabu jmn

lightveronica2: We zuchu vaaga nguo sawa sio ma sweeta