Ala!Sikuwahi shika mimba,'Esma aeleza kwanini hakutaka mimba yake mumewe

Muhtasari
  • Esma adai hajawahi avya mimba ya mumewe na hakuwahi taka kupata mimba ya Msizwa
  • Awali kwenye mitandao ya kijamii ya instagram Esma alidai kwamba aliavya mimba ya msizwa kwa maana hakuwa anampenda

Dada yake staa wa bongo Diamond Platnumz Esma Khan kwa muda sasa amekuwa talk of the town baada ya kufichua kwamba aliavya mimba ya aliyekuwa mumewe kabla ya wawili hao kutemana.

Esma na Msizwa waliachana miezi chache baada ya wawili hao kufanya harusi ya kupigiwa mfano.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram Esma alifichua kuwa wameachana na mumewe na kwamba ahangeweza kubabe au kuzalia mwanamume mtoto ambaye hampendi.

 

Baada ya Msizwa kusema Esma anapaswa kukamatwa kwa ajili ya kuavya mimba yake sasa mwanamke huyo amebadili usemi wake na kusema,

"Katika mahusiano yetu tulikuwa tunavutana na nilivyokuwa naona zile tabia zake sikuwahi shika mimba wala kuavya mimba 

Mimi ni mwanamke napenda watoto sana." Alisema Esma.

Akiwa kwenye mahojiano awali alisema kwamba Msizwa alikuwa anawatumia jumbe wadada kwenye instagram na kujisahau kuwa yeye ni mwanamume ambaye ana familia yake.