Aliyekuwa mpenzi wa Eric Omondi afichua sura ya kipenzi kipya

eric.omondi.and.chantal
eric.omondi.and.chantal

Chantal Grazioli aliyekuwa mpenzi wa mcheshi maarufu, Eri Omondi hatimaye amethibitisha kuwa ameendelea na maisha yake baada ya kuchapisha picha ya kipenzi chake kipya.

Siku chache zilizopita, Chantal almaarufu Miss Chanty alichapisha picha ya kipenzi chake lakini alikuwa ameficha uso wake, na kuwafanya mashabiki wake kuuliza maswali chungu nzima.

Picha hiyo ilimbatana na siku ambayo Eric Omondi alikuwa akifanya harusi na mwanamuziki  na mshindi wa kipindi cha 'Wife material' Carol.

Wengi walidhania kuwa alikuwa akimuonesha Omondi kuwa tayari amepata jiko lake baada ya wawili hao kutengana miaka michache iiyopita.

Baadhi ya jumbe alizopokea ni kuwa mwanaume huyo ambaye anaonekana kuwa na asili ya kigeni ni bora kuliko Omondi.

Soma baadhi ya jumbe hizo;

Oloo: Me and Erick omondi are feeling chest pains right now ❤️❤️😂😂😂

Anita Linah: Nice.. better than@ericomondi

Iamkathawrey: Perfect for each other

Japhitha: Ndo ivo sasa...ukiachwa hakuna kupreach..unasonga mbele

Angela Oronya: Baaaas sasa ndio mwafaana