Video ya siku: Willy Paul amshirikisha Miss P kwenye kibao 'Liar'

Hivi majuzi msanii Willy Paul alitangaza kuwa amemsajili msanii chipukizi Miss P katika lebo yake ya usanii, Saldido International.

Willy Paul alitangaza kuwa msanii huyo ambaye umaarufu wake bado haujatamba, ana talanta chungu nzima na ana furaha kwani anajua uwezo wake na kile ambacho amewaandalia mashabiki wake.

Jumamosi alizindua kibao kipya cha 'liar' alichomshirikisha Miss P, mwanadada aliyeumbwa akaumbika.

Wengi wamependezwa na sauti yake nyororo ya kumtoa nyoka pangoni huku wakimsifia Willy Paul kwa kukigundua kipaji hiki na kuamua kukilea.

Zifuatazo ni baadhi ya jumbe kutoka kwa mashabiki wa Pozze;

Marwa: Great Music Bro , somehow sounds like Otile !

Justus K: Mimi mnisulubu ama mnipige mawe ata mnaweza ninyonga lakini, Pozze is very good at composing his music and you cannot talk about the Kenyan music industry without mentioning his name Thanks for attending my TED Talk.

Rosaline Murugi: Other guys: Don't mind, she's just a friend, she's my cousin... Pozze; ni mama wa kuuza maboxer tu

Mugushu Selina: Every song that willy paul releases becomes my favourite song ....alafu tusisahau part ya ni mama wa kuuza boxer