'Naamini atamuonyesha kaburi la baba yake,'Mzee Abdul amwambia Mama Dangote

Muhtasari
  • Mzee Abdul asema kwamba mama Dangote hakumwambia kwamba ujauzito si wake
  • Pia alisema kwamba anaamini mama huyo atamuonyesha msanii huyo kaburi la baba yake
  • Abdul alifichua kwamba alimsaidia mama Dangote enzi hizo alipokuwa tajiri
Mzee-Abdul
Mzee-Abdul

Familia yake staa wa bongo Diamond Platnumz imekuwa kwenye vichwa vya habari punde tu mama yake alipofichua kwamba mzee Abdul si baba yake diamond.

Mama yake Diamond, alipost picha Instagram za mwanamume kwa jina Salim Idi Ny'ange, anayedai ni baba halali wa mmiliki huyo wa Wasafi Records.

Mzee Abdul ameweka wazi kwamba anatumai kwamba mama Dangote atamuonyesha msanii huyo kaburi la baba yake.

 

"Naachia yote mwenyezi Mungu, naamini kwamba mama yake ataenda kumuonyesha kaburi la baba yake, nafikiri wangeniita katika mkutano wa kifamilia ili kufichua habari hizi badala ya kuzifichua kwa umma." Abdul Alizungumza.

Mzee Abdul alikumbuka jinsi alimsaidia Mama Dangote wakati Diamond alipokuwa mchanga kwa maana hakuwa na mtu yeyote wa kumsaidia.

"Ukweli nilikuwa tajiri, nilimsaidia kifedha alikataa kunambia kwamba ujauzito si wangu kwa maana hakuwa na pesa

Alifikiria kuwa hamna mtu ambaye atamsaidia akisema ukweli ."

Mzee Abdul na Mama Dangote waliachana msanii huyo akiwa kidato cha kwanza.