Msanii Diamond adinda kuzungumzia swala la mzee Abdul kutokuwa baba yake

Muhtasari
  • Msanii Diamond adinda kuzungumzia swala la mzee Abdul kutokuwa baba yake
  • Hii ni baada ya Sandra kudai kwamba Abdul si baba yake kamili wa msanii Diamond
  • Diamond alisema swala hilo atalizungumzia wakati mwingine
Diamond Platnumz

Jamii ya staa wa bongo Diamond Platnumz kwa muda sasa imekuwa kwenye vichwa vya habari kkutoka kwa dada yake Esma hadi kwa mama Dangote.

Wiki jana mama Dangote alisema kwamba mzee Abdul si baba yake Diamond ambapo ilizua gumzo kwenye mitandao ya kijamii.

Ukweli ni kuwa Abdul si baba yake Diamond, huku akiwa kwenye Tamasha Dar-Es Salaam Tanania alidinda kuzungumzia suala hilo huku akisema atalizungumzia siu nyingine.

 

"Kila maneno yana mahala pake, tukisema tuzungumzie maneno ya kitandani hapa, sio sehemu yake

nawauliza tafadhali kaeni na swali lenu nitakuja kulizungumzia siu nyingine." Diamond Aliongea.

Mashabiki na wana mitandao walikuwa wamegonja kwa hamu msanii huyo azungumzie suala hilo na kutoa maoni yake.

Huku mzee Abdul akizungumza kuhusu jambo hilo alisema kwamba anaamini mama Dangote atamuonyesha Diamond kaburi la baba yake.

Pia alisema kwamba ,mama Dangote angemuita katika mkutano wa familia ili kutangaza jambo hilo na wala si kulitangaza kwenye mitandao ya kijamii.