Mwanahabari Lilian Muli afichua majuto makubwa maishani mwake

Muhtasari
  • Mwanahabari Lilian Muli afichua majuto makubwa maishani mwake
  • LIlian alisema kwamba alimpenda mtu lakini alimdanganya
Lillian-Muli-new-look-696x418
Lillian-Muli-new-look-696x418

Kupata mtu ambaye anakupenda na ambaye hatasaliti upendo wako au moyo wako katika karne hii ni ngumu sana.

Ndio utakuwa katika uhusiano wa kimapenzi lakini utanmpata mpenzi wako yuko na mpango wa kando nje.

Huku mwanahabari wa runinga ya Citizen Lilian Muli alisema majuto yake makuu ni kumpenda mtu ambaye alimdanganya.

 
 

KUpitia kweye ukurasa wake instagram kipindi cha maswali shabiki mmoja alimuuliza majuto yake makuu katika maisha yake ni yapi na kisha alimjibu kuwa ni kumpenda mtu ambaye alimdanganya.

Lilian Muli
Lilian Muli

Shabiki alimuuliza,"Majuto makubwa."

Lilian Muli naye alijibu haya;"Kumpenda mtu ambaye ni mdanganyifu."

Pia Lilian alifichua kwamba hana mpenzi kwa sasa, hii ni baada ya mashibiki mwingine kumuuliza kama yuko katika uhusiano wa kimapenzi.

Awali upitia kwenye mitandao ya kijamii mwanahabari huyo aliwashauri mashabiki wake kuwa wanapaswa kuwa na kiwango cha maisha na kukaa katika kiwango hicho bila huruma yeyote.