Wazazi wangu waliaibika kunilea-Letoya Johnstone afunguka

Muhtasari
  • Letoya Johnstone azungumzia maisha yake na wazazi wake huku akisema kwamba hajawahi kuwa katika uhusiano wa kimapenzi
Letoya Johnstone
Image: Radiojambo

Letoya Johnstone akiwa kwenye mahojiano na Radiojambo na ambaye alizaliwa kama mwanamume lakini alikuwa na hisia za kuwa mwanamke alifichua changamoto ambazo amekuwa akipitia.

Letoya alisema kwamba licha ya watu kumuogopa kwa maana kwa sura ya wengi yeye ni mwanamume amejikubali jinsi alivyo.

Pia alifunguka na kusema kwamba wazazi wake waliaibika kumlea.

 
 

"Nikiwa mchanga nilipenda masomo sana, lakini sikukuzwa kama mvuvi kwa maana wazai wangu walikuwa wavuvi

Mimi ni mwanamke, lakini nilizaliwa mwanamume, ilhali vitendo na mafikira yangu ni ya mwanamke, yaani nilizaliwa kwa mwili ambao si wangu

Watu wanahukumu jinsi ulivyo, na wala hawaoni ndani yako,wazazi wangu walipatwa na aibu kunilea walipogundua kuwa ikira zangu niza mwanamke

watu wengi wanatufananisha na watu wenye jinsia mbili na mashoga." Alizungumza Letoya.

Pia alisema kwamba watu humuogopa ndio maana hajawahi kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi.