Kama Mungu hutanibariki na BMW i8 nitajiumiza-Ringtone amtishia Mungu

Muhtasari
  • Ringtone amtishia Mungu kwa mara nyingine na kusema kwamba atajiumiza kama Mungu hatambariki na BMW i8

Msanii Rngtone Apoko kwa mara tena amewaacha mashabiki wake tena na midomo wazi baada ya kumtishiaMungu na kusema kama hatambariki na gari ya aina ya BMW i8 atajiumiza.

Mapema wiki hii msanii huyo alimtishia Mungu na kusema kwamba asipo mbariki na gari hilo baada ya kfunga na kuomba kwa siku 40 ataacha kumtumikia.

Pia aliendelea na kusema kwamba hawezi tumikia Mungu abaye hajibu maombi yake.

 

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagrma Ringtone alisema kwamba imebaki tu siku 26 ili amalize siku zake za kufunga na kuomba.

"Mungu kama hutanibariki na hii gari la aina ya BMW i8 baada ya siku 26 naapa nitajiumiza, Mungu wangu ni tajiri akiwa mbinguni, namshukuru kwa kunipa gari ya milioni 26

Lakini Mungu wangu sasa ni tajiri anapaswa kunipa kile nataka, Mungu wangu hataniaibisha." Rigtone Aliandika.

KIlichowashangaza mashabiki ni je atatimiza alichosema msanii huyo kwa mara ya kwanza kwamba ataacha muziki wa injili au atatimiza ili amelisema la mwisho kwamba atajiumiza?