(+Video)Acheni kuniambia mambo ya kuzaa mume wangu alikataa tuongeze mtoto-msanii Nyota Ndogo

Muhtasari
  • Nyota Ndogo aeleza sababu ya kutomzalia mumewe mzungu huku akisema walionao wametosha
  • Mnamo Machi 2020, muimbaji huyo alisimulia namna alihangaika kumzalia Nielsen watoto
83532576_627204834703118_8454513908795708531_n
83532576_627204834703118_8454513908795708531_n

Msanii Nyota Ndogo kwa mara ya kwanza ameweka mambo wazi kwa nini hajawahi mzalia mume wake mzungu.

Nyota Ndogo alipakia video kwenye ukurasa wake wa instagram video akiimba wimbo wake ambao unazungumzia ndoa na watoto na kufichua kuwa mume wake alikataa kuongeza watoto. 

Msanii huyo alidai ya kwamba mume wake alikataa waongeze mtoto mwingine na tayari yuko na wajukuu.

nyota ndogo
nyota ndogo

Pia Nyota alisema kando na wanawe wawili, tayari mume wake ana watoto wengine watatu na wajukuu hivyo wanatosha.

"Mume wangu alikataa tuongeze mtoto. Alisema amekua mtu mzima na yupo na wajukuu na akiweka watoto wake watatu na wangu wawili tupo na watano so plzz acheni kuniambia mambo ya kuzaa ama nimzalie ama wengine kuniambia hooo hutaki kumzalia kwakua nimzee. At list jibu munalo. Naaa munajua kama wazungu hawataki kuzaa ufanya nini sio? Haya basi." Aliandika Nyota.

Nyota ni msanii wa kutoka mkoa wa pwani, alifahamika sana kupitia kwa kibao chake cha Watu na Viatu.

Mnamo Machi 2020, muimbaji huyo alisimulia namna alihangaika kumzalia Nielsen watoto, kutokana na hamu yake ya kutaka kuwa na familia kubwa.

Katika mahojiano na Radio Jambo, mama huyo wa watoto wawili alisema aliwatembelea madaktari wa kila aina lakini wawili hao walishindwa kupata watoto.