Mke wangu alikuwa analeta wanaume nikiwa kwenye kiti cha walemavu-Mwanamume asimulia

Muhtasari
  • Mwanamume aeleza jinsi aliteseka akiwa mikononi mwa mkewe alipokuwa mgonjwa
  • Licha ya wawili hao kuwa mume na mke mkewe alikuwa anawaleta wanaume wengine kwa nyumba

Kuna baadhi ya wanawake ndio watakupenda kwa ajili ya pesa na mali yako, bali ukipatwa na shida kidogo utaona upande ule mwingine wao ambao hawakuwa wamekuonyesha.

Mwanamume mmoja aliwaacha wengi wakiwa wamepigwa na butwaa baada ya kusimulia jisi mke wake alimtesa alipokuwa mgonjwa.

"Mke wangu alikuwa anawaleta wanaume nyumbani nikiona nilipokuwa  kwenye kiti cha vilema,wakati huyo nilikuwa nimehusika kwa ajali

Nilipokuwa namuuliza alikuwa ananiambia nisimame nimpige au nifukuze wanaume hao

Jambo nzuri mimi nilimsamehe kutoka kwa moyo wangu." Alieleza Mwanamume huyo.

Baada ya mwanamjme huyo kufungua roho, mwanamke mmoja naye aliamua kufungua roho na kusema haya.

"Nikiwa kwenye ndoa yangu ya awali, mume wangu alikuwa ananitesa, licha ya yetu kufunnga ndoa kwa kanisa, nikiwa mgonjwa mwanamume huyo alikuwa anatarajia niamke nikafanye kazi nilipe nyumba na hata ni nunue chakula

Lakini namshukuru Mungu kwa maana sasa niko na furaha baada ya kutoka kwenye ndoa hiyo."