Si umemove on haraka! Mashabiki wamwambia Mulamwah baada ya kupakia picha akiwa na mwanamke

Muhtasari
  • Mchekeshaji Mulamwah aambiwa haya na mashabiki baada ya kupakia picha akiwa na mwanamke
Mulamwah 2
Mulamwah 2

Mchekeshaji Mulamwah amewasha mitandao ya kijamii baada ya kupakia picha akiwa na mwanamke huku wakiwa na furaha.

Kulingana na Mulamwah alikuwa na wakati mwema na mwanamke huyo ambaye inadaiwa ni mpenzi wake.

Baada ya kupakia picha hiyo aliandika ujumbe huku akimsifia mwanamke huyo.

 

"Konki yuko sawa, tulieni nyinyi nyote."Mulamwah Aliandika

Mashabiki walijaza sekta ya maoni ya hisia tofauti, huku wengi wakimwambia ameendelea na maisha kwa haraka sana baada ya kuachana na mpenzi wake wa awali.

Hizi hapa hisia za mashabiki;

mylee_staicey: Heeh🙆🏾‍♀️Si ume move on harakaaa🤣😂Nairobiiiiiiiii😂

Zainabuzeddy: Diamond wa Kenya 😂😂😂😂

chriskirwa: Hii ni Sawa Bora Asikuwe Private Investigator 😎🚶🏾‍♂️🚶🏾‍♂️ #NapitaTu

_pokot_niccur: Kifaa kipyaa atleast ume blend😂😂😂😂

 

msaniibabji: Konki valentine's inakuom❤️❤️❤️❤️❤️🙏

westkid___: Umeamua kumuanika 💥