Ringtone apeana sababu yake ya kutaka Mungu ambariki na BMW i8
Wengi waliachwa na maswali chungu nzima haswa kwanini msanii wa nyimbo za injili Ringtone Apoko anahitaji gari la aina na BMWi8, huku akimtishia Mungu.
Ndio tunajua kwaba Ringtone anapenda kutafuta kiki lakini wakati huu alionekana kuwa na tamaa ya kutaka gari hilo.
Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram msanii huyo alitangaza kuwa anafunga na kuomba kwa siku 40 na kama Mungu hatampa gari ilo ataacha kuwa msanii wa nyimbo za injili.
Baada ya siku chache pia aliandika ujumbe huo na kusema kwamba atajiumiza MUngu asipotimiza ombi lake.
Mashabiki,marafiki walishindwa kwanini Ringtone anamtishia Mungu wala usitie shaka soma sababu yake ya kutaka gari hilo.
"Hii hapa sababu kwanini Mungu anapaswa kunibariki na BMW i8 ama niacha usanii wa nyimbo za injili
Ni kwa sababu sijawahi sheherekea siku yangu ya kuzaliwa baada ya baba yangu kuaga dunia nikiwa na miaka 5, alafu nyanya yangu akaaga baada ya mama yangu kuniacha mitaani
Aliniacha nikiwa na miaka 7 nimekulia mitaani, ambapo nilikataliwa, lakini nikaanza kuimba nyimbo za injili na kuhubiri neno ambapo wengi wameokoka kwa ajili yangu
Hili gari litaenda kunifanya nisahau mambo ambayo nimepitia maishani tafadhali nisaidieni kuomba vyema." Aliandika Ringtone.
Je ushauri wako ni upi kwa msanii huyu?