'Sio lazima uelewe maisha ya watu,'Zari Hassan ampa shabiki bonge la jibu aliposema haya kuhusu mwanawe

Muhtasari
  • Zari Hassan ampa shabiki boonge la jibu, baada ya kumkejeli mwanawe Tiffah
  • Zari amekuwa akiwapa wakosoaji wake majibu vipasavyo
zari
zari

Kwa muda sasa Zari Hassan na mama wa watoto wake msanii Diamond amekuwa akipokea kejeli na ukosoaji mkubwa kutoka kwa mashabiki wake wa jinsi uwavalisha wanawe.

Kejeli za mashabiki hazijakuwa zikimnyamazisha ari bali amekuwa akiwajibu jinsi wameanza mazungumzo.

Pia amekuwa akiwaambia mashabiki na wakejeli wake sio lazima wajue na kufahamu jinsi vile watu wanaishi maisha yao.

Aliongeza na kusema shida na watanzania hudhani kwamba wanawajua watu ndani na nje kulngana na picha ambazo hupakia kwenye mitandao ya kijamii ilhali hawajui chochote.

Screenshot-from-2020-08-06-10_05_10
Screenshot-from-2020-08-06-10_05_10

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram alipakia picha akiwa na mwanawe Tiffah,huku mmoja wa mashabiki wake akisema kwamba hajaelewa jinsi Tiffah amevalia hasa ndala alilokuwa amevalia.

“But Hiyo ndala ya Tiffah Cjaelewa @Zarithebosslady."

Kwa haraka Zari naye alimjibu haya;

"Sio lazima uelewe Maisha yawatu kwa picture moja. Ilo ndo tataizo la waswahili/Wabongo.Huwa mnafikiria mnajua watu nje na ndani kupitia kwa picha moja tu. Smh! labda aliziomba kutoka kwangu au aliomba saluni alipokuwa labda labda… see there is always so many reasons lakini nyinyi, tukiwapa picture moja tu, you have it all figured out. Smh! Mnachosha mxuiii”.