Si lipishi uzinduzi wa albamu yangu elfu 50 ili kupata pesa zangu zilizopotea-Rose Muhando aweka mambo haya wazi

Muhtasari
  • Msanii Rose Muhando aeleza kwanini analipisha elfu 50, katika uzinduzi wa albamu yake
Rose Muhando

Akiwa kwenye mahijiano na Radiojambo msanii wa nyimbo za injili kutoka Tanzania Rose Muhando alizungumzia kwanini analipisha elfu 50,000 katika uzinduzi wa albamu yake.

"Nilipoitwa na Mungu aliniambia nimjengee nyumba, hizo pesa nalipisha katika uzinduzi wa albamu yangu si kwa ajili  nipate pesa zangu

Mimi nimetoka kwa familia maskini sana na wala sina haja ya pesa, lakini ni za kumjengea Mungu kanisa." Alisema Muhando.

Baada ya Rose Muhando kuweka tangazo kwenye mitandao ya kijamii kwamba uzinduzi wake wa albamu utakuwa eneo la Villa Rosa Kempinski hotel in Nairobi, mashabiki na wana itandao hawakushangazwa na eneo la hafla hiyo bali walishangazwa na pesa ambazo kila mtu anapaswa kulipa ili kuhudhuria hafla hiyo.

MUhando alieleza kwanini wasanii wa nyimbo za 'Secular' wanatamba sana kuliko wasanii wa nyimbo za injili.

"Kusema ukweli sisi wasanii wa nyimbo za injili hatujitumi sana katika kazi yetu kama wasanii wa nyimbo za secular,"