Utapoteza nini kama uhusiano wangu hutadumu? Zari awauliza wakosoaji

Muhtasari
  • Zari Hassan awajibu wakosoaji wake wanaodai uhusiano wake hutadumu
  • Kupitia kwenye mitandao yake ya kijamii Zari alifichua kwamba ana mshikaji
Zari Hassan
Zari Hassan

Mitandao ya kijamii siku chache zilizopita iliwaka moto baada ya mwanasosholaiti Zari Hassan kufichua kwamba ana mshikaji.

Baadhi ya wanamitandao walisema kwamba uhusiano huo hautadumu na kuwa kuna mtu atalia baada ya uhusiano huo kuisha.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram Zari aliwaambia wakosoai wake hawatapoteza chochote uhusiano wake ukiisha.

 

"Watu wengi wenye huzuni watataka kukuona katika kikundi chao cha WhatsApp. Usinihesabie katika kitengo hicho ombaomba.

Nakataa kuwa mmoja wenu. Furaha inaishi hapa. Ikiwa inaisha kwa kilio na  machozi basi, wewe kama mtu utapoteza nini?"aliandika Zari Hassan.