(+Video)Tuliachana na mpenzi wangu kwa maana hakuwa na uwezo wa kunipa mtoto-Wema Sepetu afichua

Muhtasari
  • Wema Sepetu afichua aliachana na mpenzi wake kwa ajili ya kutokuwa na uwezo wa kumpa mtoto
  • Pia muigizaji huyo alisema kwamba alificha uhusian wake lakini hatimaye akamtambulisha mpenzi wake hadharani
Wema Sepetu
Wema Sepetu

MUigizaji Wema Sepetu akiwa kwenye mahojiano alieleza na kuweka mambo wazi kwamba aliachana na mpenzi wake kwa sababu moja au nyingine.

Lakini sababu kuu ya kuachana naye ni ipi?

Wema alisema kwamba licha yake kutarajia mengi kutoka kwa mpenzi wake waliachana kwa maana hakuwa na uwezo wa kumpa mtoto.

 

"Kwa kweli nilikuwa nikitarajia kuolewa naye lakini jambo moja au tuseme moja ya sababu ambazo zilisababisha kuachana kwetu ni kutokuwa na uwezo wa kunipa watoto.

Ilikuwa mbaya kwangu kwa sababu kama mwanadamu, nilikuwa na matarajio yangu. na nilikuwa nikitarajia mapenzi yetu yangechipuka na kuimarishwa na ngono na mwishowe mtoto," Alisema Wema.

Pia alifichua kwamba amekuwa akificha uhusiano wake awali, ilhali mwaka wa 2020 alimuweka mchumba wake hadharani kabla ya kuachana.

'' Nimekuwa nikificha sana juu ya uchumba wangu hivi karibuni. Watu walijaribu kujua nilikuwa nikichumbiana na nani au ninampenda nani kwa sasa.

Mnamo mwaka wa 2020 nilikuwa katika uhusiano na mtu huyu na niliweka hadharani katika mahojiano kadhaa. "Wema alisema.

Wema Sepetu alisema kabla ya Kanumba kuaga dunia alikuwa anampigia simu ili wapatane bali hakuweza kwa maana alikuwa na kazi nyingi,lakini hatimaye waliweza kupatana.

'' Ninahisi kama Kanumba alinilaani. Hii ni kwa sababu alitaka sana kuniona, angeita kila siku wiki mbili kabla ya kifo chake

 
 

Tulipaswa kukutana lakini tulikuwa na shughuli nyingi hatukuweza. Aliita kama mara nne lakini hatukuweza kukutana

Hatimaye tulikutana huko Bilcanas, aliniambia, angalia ni wapi tutakutana,"